Al-Itrah Foundation


Salam alaikum.


Nimatumaini yangu u mzima na unaendelea vema na saumu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani. Sisi hatujambo. Napenda kukufahamisha kuwa kile kitabu cha upotofu wa mawahabi kimeleta athari nzuri sana kwa watu shia na suni. Masuni ndio zaidi wamekifurahia sana na kila siku wanakuja kwangu kuulizia nakala ya kitabu hicho. Naomba sana utupatie box hata kumi kama kuna uwezekano. 

Pia ni vizuri kitabu hicho kichapishwe tena nakala nyingi kwani kinahitajika sana na hasa kwa ndugu zetu masuni ambao hawana hoja za kutosha kukabiliana na mawahabi kwani hiyo ni silaha tosha ya kutetea na kulinda imani yao.


Natanguliza shukrani zetu za dhati kwa msaada wenu kwetu na kwa Uislamu kwa ujumla.

Wasalaam
Abdul karim – Singida
Madrasatul Wahda