TCRA kuzifungia Simu Bandia.


 

 

 

TCRABOSSMamlaka  ya Mawasiliano nchini (TCRA) imetoa miezi sita kwa watumiaji wa  simu za mkononi ambao wanatumia simu bandia kuachana nazo la sivyo watazifungia.

 

Pia TCRA imetoa mwongoza kwa watumiaji wa simu hizo kuzihakiki simu zao kama ni harali, ambapo watumiaji wanatakiwa kupiga simu*#06# kasha zitatokea namba mara baada ya kupiga na kinachotakiwa ni kuzichukua namba hizo kisha kwenda kwenye sehemu ya kuandika ujumbe mfupi na kuziandika namba hizo,

 

Ksha unatuma ujumbe wa namba hizo  kwenda  kwenye namba maalum 15090  na utapata matokeo  kamili kuhusu uhalali wa simu ikiwemo pia kuzisajili.

 

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam  na mkurugenzi mkuu wa (TCRA) Dkt Ally Simba  wakati akiutambulisha, mfumo mpya wa rajisi ya namba za utambulisho wa simu za kiganjani, kwenye makao makuu ya Mamlaka hiyo yaliopo Jijini Dar es salaam,ambapo amesema  nia ya TCRA ni kuziondoa simu zote bandi katika mfumo wa utumiaji wa simu.

 

Pia  amesema mfumo huo utasaidia kuongeza usalama mtandaoni kwa watumiaji wa simu kwa madai kuwa simu zote za mkononi  zitakuwa zimejulikana kutokana na kusajiliwa kwenye mfumo huo na kuzuia matumizi ya simu zisizokuwa na viwango hivyo kusaidia kuepuka madhara yatokanayo na simu zisizokuwa bora na stahiki.

2 Comments

  1. Amon Lugoye says:

    Hongera sana TCRA kwa kazi nzuri mnayoifanya katika nyanja hii ya mawasiliano, na hoja kwenu mtupe ufafanuzi wa kina juu ya udhibiti wa simu bandia. kuna simu toka nchi maarufu kwa utengenezaji zana nyingi za kielektroniki mfano Mimi natumia TECNO Y4 unapoingiza ile namba kupata imei zinakuja namba mbili nafikiri kwa sababu ya line mbili, hoja yangu imei ya kwanza ninapoingiza inaniletea ujumbe kuwa ni TECNO Y4, na ninapoingiza lmei ya pili inaonyesha simu hii no Samsung, ukweli no UPI juu ya simu hii maana kila imei ina matokeo tofauti, haki ya umiliki hapa ni ipi na zoezi la kuzima litakapofika ni ipi itazimwa?

Leave a Comment