Category: Habari za Kitaifa

Lissu Kortini, Aenda Rumande.

Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya Chadema, Tundu Lissu (pichani) ataendelea kusota rumande hadi Julai 27, mwaka huu akisubiri uamuzi wa mahakama kuhusu pingamizi la dhamana. Alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam jana na kusomewa mashitaka ya kutoa lugha ya uchochezi. Mshitakiwa alikana mashitaka hayo na upande wa mashitaka ulidai [&hellip

JPM Amfagilia Kafulila IPTL.

Rais John Magufuli amesema kukosa uzalendo kwa baadhi ya watendaji waandamizi wa serikali, ndiko kulikosababisha kuitumbukiza nchi kwenye ufi sadi wa sakata la Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL na kuitia hasara kubwa serikali. Akizungumza muda mfupi baada ya kuzindua mradi wa maji katika Kijiji cha Nguruka, Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma, Rais Magufuli amempongeza [&hellip

Majaliwa Amtumbua DED, Wengine 3.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, Eliseyi Mgoyi pamoja na maofi sa wengine watatu kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za umma. Pia amemuagiza Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Songwe, Damian Sutta kuwakamata na kuanza kuwachunguza [&hellip

‘Majambazi’ Dar Wapewa Siku 7 Kujisalimisha Polisi.

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limetoa siku saba kwa majambazi wote waliowahi kutumikia vifungo na kuachiwa kwa kumaliza vifungo au rufaa, wajisalimishe kwa Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu. Kauli hiyo ilitolewa jijini hapa na Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu, Lucas Mkondya wakati akizungumza na waandishi wa habari. Mkondya alisema lengo [&hellip

Wakimbizi Rudini Burundi –JPM.

Rais John Magufuli amempongeza Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi kwa juhudi zake za kusimamia amani nchini mwake. Ametoa ushauri kwa wakimbizi wa Burundi hapa nchini, kuitikia wito wa Rais wao, aliyewataka warudi nchini mwao kwenda kulijenga Taifa lao kwa kuwa hali ni shwari. Rais Magufuli aliyasema hayo jana kwenye mkutano wa hadhara, uliofanyika kwenye Uwanja [&hellip

Manji Ashindwa Kuhudhuria Kortini.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kuwa amepata taarifa kutoka kwa daktari wa Magereza kwamba mfanyabiashara Yusuf Manji (41), amepelekwa katika Hospitali ya Gereza la Keko kwa kuwa hali yake sio nzuri. Katuga alidai hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kesi hiyo ilipokuja [&hellip

Jaji Mstaafu Wa Mahakama Kuu, Upendo Msuya Afariki Dunia.

Aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu ambaye amejiuzulu hivi karibuni, Upendo Msuya amefariki jana Julai 19 baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa kiharusi. Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu, mjomba wa marehemu, Niva Mbaga amesema kwamba marehemu amefariki akiwa Hospitali ya Kairuki alipokuwa amelazwa. Amesema kwamba shughuli za mazishi zinafanyika nyumbani kwa marehemu [&hellip

JPM: Sina Utani Matumizi Ya EFDs.

Rais John Magufuli ametoa siku 14 kwa wamiliki wa vituo vya mafuta nchini, kuhakikisha kwamba wanafunga mashine za kielektroniki za kutolea risiti (EFDs) na kuonya watakaoshindwa kufanya hivyo watahatarisha biashara zao. Ametoa agizo hilo jana alipohutubia mkutano wa hadhara mjini Biharamulo mkoani Kagera wakati wa kuzindua barabara ya Kagoma – Biharamulo – Lusahunga yenye urefu [&hellip

Makamu Wa Rais Aongoza Mamia Kuaga Mwili Wa Merehemu Linah.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi Samia Suluhu Hassan amewaongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa aliyekuwa mke wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, Bi. Linah George Mwakyembe katika Kanisa la KKKT lililopo Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam. Wakati wa kuaga mwili wa marehemu Linah, [&hellip

Watoto Wanne Wamefariki Dunia Baada Ya Kujifungia Kwenye Gari.

Watoto wanne wamefariki dunia baada ya kujifungia kwenye gari kwa muda mrefu huko katika maeneo ya kidongo Chekundu Mjini Zanzibar. Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tukio hilo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Hassan Nassir amesema tukio hilo lilitokea hapo jana katika maeneo ya kidongo Chekundu ambapo watoto hao wamekutwa [&hellip