Category: Habari za Kitaifa

Magufuli- Makonda Alipe Kodi Ya Makontena.

Magufuli- Makonda Alipe Kodi Ya Makontena.

Rais Dk. John Magufuli amesema makontena 20 yaliyoingizwa nchini kwa jina la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda lazima yalipiwe kodi. Ameagiza viongozi wote nchini kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria na wasimamie ipasavyo matumizi ya rasilimali za umma kwa maslahi ya wananchi. Kwa mujibu wa Rais Magufuli, Waziri wa Fedha na [&hellip

Mpasuko Kamati Ya Bunge Ya Bajeti.

Mpasuko Kamati Ya Bunge Ya Bajeti.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Hawa Ghasia na Makamu wake, Jitu Soni wamejiuzulu nyadhifa zao jana, Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai amethibitisha. Aidha, wajumbe wa kamati hiyo walikutana saa 11 jioni kwa ajili ya kuchagua viongozi wengine wa kushika nyadhifa hizo. Mwenyekiti mpya aliyechaguliwa ni George Simbachawene ambaye ni Mbunge wa Kibakwe mkoani [&hellip

RC Awatoa Hofu Mlipuko Ebola.

RC Awatoa Hofu Mlipuko Ebola.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo amewatoa hofu wakazi wa mkoa huo kuwa ugonjwa wa ebola haujaingia huko. Amesema, hadi sasa hakuna mtu yeyote aliyethibitishwa au kuhisiwa kuwa na ugonjwa huo mkoani humo. Wangabo amesema, mkoa huo umejizatiti kuimarisha ufuatiliaji na kutekeleza mikakati ya udhibiti ili ugonjwa huo usiingie mkoani humo. Amesema kwa njia [&hellip

Tanzania, Uganda Zaingia Makubaliano Mapya.

Tanzania, Uganda Zaingia Makubaliano Mapya.

Tume ya Kudumu ya Pamoja kati ya Tanzania na Uganda, imekubaliana kuongeza kasi ya ushirikiano baina ya mataifa hayo mawili katika mkutano wa pili baina ya pande hizo, uliomalizika jana katika mji wa Munyonyo nchini Uganda. Pamoja na mambo mengine, tume hiyo ilijadili na kutathimini utekelezaji wa makubaliano ya ushirikiano, yaliyofikiwa baina ya pande mbili [&hellip

Wakili Kesi Ya Uchochezi Ya Kina Mbowe Ajitoa.

Wakili Kesi Ya Uchochezi Ya Kina Mbowe Ajitoa.

Wakili wa kujitegemea, Jeremiah Mtobesya anayewatetea vigogo tisa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), akiwemo Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe (pichani), wanaokabiliwa na mashitaka ya kufanya mkusanyiko usio halali katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, amejitoa katika kesi hiyo. Wakili Mtobesya alifanya maamuzi hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri baada ya upande [&hellip

Tanzania yakabiliwa na hatari kubwa ya mlipuko wa homa ya Ebola.

Tanzania yakabiliwa na hatari kubwa ya mlipuko wa homa ya Ebola.

Waziri wa afya wa Tanzania Bibi Ummy Mwalimu amesema, Tanzania inakabiliwa na hatari kubwa ya kutokea kwa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola, ambao umesababisha vifo vya watu 50 kati ya wagonjwa 91 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC Bi. Mwalimu amesema, kwa mujibu wa takwimu mpya za shirika la afya duniani WHO, mlipuko mpya [&hellip

Majaliwa Abana Wakurugenzi, Ma- Ded.

Majaliwa Abana Wakurugenzi, Ma- Ded.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewaagiza wakuu wa wilaya na wakurugenzi kusimamia utendaji kazi katika maeneo yao ili kuendana na kasi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli. Majaliwa ametoa agizo hilo juzi alipokuwa akizungumza na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali pamoja na watumishi wa umma katika ziara [&hellip

Waziri Mwakyembe Atua Geita Kwa Ajili Ya ‘Jukwaa La Fursa Za Biashara’.

Waziri Mwakyembe Atua Geita Kwa Ajili Ya ‘Jukwaa La Fursa Za Biashara’.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amewasili Mjini Geita leo (Jumatano) na kutembelea mabanda ya washiriki wa Jukwaa la Fursa za Biashara lililoandaliwa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali ya Tanzania Standard Newspapers (TSN) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita. Kabla ya kuwatembelea wafanyabiashara hao na kujionea [&hellip

Jafo Aagiza Udhibiti Wizi Wa Dawa.

Jafo Aagiza Udhibiti Wizi Wa Dawa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo amesema chini ya asilimia 30 ya vituo vya afya ndivyo vimefunga mifumo ya kielektroniki. Amewaagiza waganga wakuu wa mikoa, wilaya na wafawidhi kutimiza wajibu wao na kuhakikisha wanasimamia ipasavyo rasilimali fedha na uvujaji wa dawa katika hospitali na vituo vya [&hellip

5 Wafa Ajalini Wakisafirisha Samaki.

5 Wafa Ajalini Wakisafirisha Samaki.

Watu watano wamekufa wilayani Tarime na Rorya mkoani Mara, baada ya gari walilokuwa wakisafiria lililokuwa limesheheni magunia ya samaki likiwa kwenye mwendo mkali, kugonga nguzo ya karavati na kupinduka. Ajali hiyo imepoteza maisha ya dereva na mmiliki wa gari hilo aina ya Probox lenye namba za usajili T 258 BGB. Watu wengine watatu wamejeruhiwa na [&hellip