Articles By: admin

Nduli wa mauaji ya Waislamu CAR apandishwa kizimbani ICC.

Nduli wa mauaji ya Waislamu CAR apandishwa kizimbani ICC.

Alfred Yakatom, ambaye wakati fulani alijulikana kwa jina la Rambo kutokana na kufanya mauaji makubwa dhidi ya Waislamu huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC akikabiliwa na mashtaka 14 ya jinai za kivita na jinai dhidi ya ubinadamu. Wakili wa mtuhumiwa huyo ambaye ni maarufu kwa kutesa [&hellip

UN: Idadi ya watu waliouawa katika mapigano baina makundi hasimu CAR imeshafikia 60.

UN: Idadi ya watu waliouawa katika mapigano baina makundi hasimu CAR imeshafikia 60.

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, idadi ya watu waliouawa katika mapigano baina ya makundi hasimu huko Jamhuri ya Afrika ya Kati imeshafikia 60. Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa, mapigano baina ya kundi la Seleka na hasimu wake mkubwa genge la Kikristo la Anti Balaka yaliyozuka tarehe 15 Novemba katika mji wa Alindao [&hellip

Watu 7 wauawa katika hujuma ya Boko Haram nchini Niger.

Watu 7 wauawa katika hujuma ya Boko Haram nchini Niger.

Watu waliojizatiti kwa silaha wanaoaminika kuwa na mfungamano na genge la kigaidi na ukufurishaji la Boko Haram wameshambulia kampuni ya kuchimba visima vya maji ya Ufaransa ya Foraco kusini mashariki mwa Niger na kuua watu wasiopungua saba. Ofisa wa serikali katika kijiji cha Toumour mkoani Diffa ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa, wafanyakazi sita [&hellip

Ethiopia yamteua mwanamke mpinzani kuongoza Tume ya Uchaguzi.

Ethiopia yamteua mwanamke mpinzani kuongoza Tume ya Uchaguzi.

Bunge la Ethiopia limemuidhinisha kiongozi mashuhuri wa upinzani aliyekuwa akiishi uhamishoni, Birtukan Mideksa kuwa mkuu mpya wa Tume ya Uchaguzi nchini humo. Waziri Mkuu wa nchi hiyo Ahmed Abey amemtaja mwanasiasa huyo aliyerejea nchini Ethiopia wiki chache zilizopita akitokea Marekani, kuwa ni shakhsia anayeheshimu mfumo wa sheria, huru na asiyeegemea upande wowote, na ni mwenye [&hellip

Askari wapatao 100 wa Nigeria wauawa katika shambulio dhidi ya kituo cha jeshi.

Askari wapatao 100 wa Nigeria wauawa katika shambulio dhidi ya kituo cha jeshi.

Askari wapatao 100 wa jeshi la Nigeria akiwemo afisa wa ngazi za juu wa jeshi hilo wameuliwa katika shambulio dhidi ya kituo cha jeshi, ambapo duru za usalama zinasema, limefanywa na kundi linalojiita Dola la Kiislamu Afrika Magharibi. Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na duru za usalama, shambulio hilo lilifanywa siku ya Jumapili dhidi ya [&hellip

UN yaipongeza Uganda na Chad kwa kuwasomesha watoto wakimbizi.

UN yaipongeza Uganda na Chad kwa kuwasomesha watoto wakimbizi.

Umoja wa Mataifa umezipongeza serikali za Uganda na Chad kwa kuwasomesha watoto wakimbizi katika shule za taifa na kuwafanya wawe na utangamano. Hayo yalisemwa jana na Manos Antoninis, Mkurugenzi wa Ripoti ya Tathmini ya Elimu Duniani ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ambaye ameongeza kuwa, jitihada za nchi mbili [&hellip

Un yalaani ukandamizaji wa askari wa serikali nchini Cameroon.

Un yalaani ukandamizaji wa askari wa serikali nchini Cameroon.

Kamisheni Kuu ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imelaani kuongezeka machafuko katika maeneo ya kusini magharibi na kaskazini magharibi mwa Cameroon na kuvilaumu vikosi vya serikali kuwa ndiye mhusika mkuu wa machafuko hayo. Ravina Shamdasani, msemaji wa Kamisheni Kuu ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa amesema kuwa umoja huo una wasiwasi [&hellip

Hujuma ya anga ya Marekani yaua 37 nchini Somalia

Hujuma ya anga ya Marekani yaua 37 nchini Somalia

Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) na Kamandi ya Jeshi la Marekani barani Afrika (AFRICOM) zimedai kuwa mashambulizi ya anga ya wanajeshi wake yamefanikiwa kuangamiza wanachama 37 wa kundi la kigaidi na kitakfiri la al-Shabaab nchini Somalia. Marekani inadai kuwa imeshirikiana na jeshi la Somalia katika hujuma hiyo iliyolenga maficho ya wanamgambo hao wa kitakfiri [&hellip

Boko Haram laua wakulima wengine tisa Jimbo la Borno.

Boko Haram laua wakulima wengine tisa Jimbo la Borno.

Wakulima tisa wameuliwa na wengine 12 wametekwa nyara katika shambulio jipya lililofanywa na kundi la kigaidi na ukufurishaji la Boko Haram katika mji wa Maiduguri, kaskazini mashariki mwa Nigeria. Viongozi katika jimbo la Borno wamesema, watu wengine watatu pia wamejeruhiwa katika shambulio lililofanywa na kundi hilo la kigaidi dhidi ya kijiji kimoja kilichoko kilomita tano [&hellip

HRW: Misri inawazuilia kusikojulikana makumi ya watetezi wa haki za binadamu.

HRW: Misri inawazuilia kusikojulikana makumi ya watetezi wa haki za binadamu.

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema vyombo vya usalama nchini Misri vimewatia nguvuni na kuwazuilia kusikojulikana makumi ya watetezi wa haki za binadamu tangu mwezi uliopita wa Oktoba hadi sasa. Michael Page, Naibu Mkurugenzi wa shirika hilo katika eneo la Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika amesema leo Jumapili [&hellip