Articles By: admin

Waziri Mkuu wa Ethiopia afikia makubaliano na wanajeshi.

Waziri Mkuu wa Ethiopia afikia makubaliano na wanajeshi.

Abiy Ahmed Waziri Mkuu wa Ethiopia jana alifikia makubaliano na mamia kadhaa ya wanajeshi wa nchi hiyo waliofika ofisini kwake wakidai nyongeza ya mishahara; ambapo wanajeshi hao walikubaliwa kumuona Waziri Mkuu huyo. Habari zinasema kuwa mkutano wa pande mbili hizo ulimalizika kwa kufikiwa makubaliano. Sambamba na kudai nyongeza ya mishahara, wanajeshi hao pia walimataka Waziri [&hellip

Al-Shabaab ya Somalia yaua 5 kwa tuhuma za ujasusi.

Al-Shabaab ya Somalia yaua 5 kwa tuhuma za ujasusi.

Kundi la kigaidi na kitakfiri la al-Shabaab la Somalia lenye mfungamano na mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda limewaua kwa kuwamiminia risasi watu watano kwa tuhuma za kufanya ujasusi kwa niaba ya vyombo vya kiintelejensia vya Marekani, Uingereza na Somalia. Genge hilo la kitakfiri kupitia radio yake ya Andalus limethibitisha kutekeleza hukumu hiyo jana Jumanne katika [&hellip

Magaidi wa Boko Haram waua wanajeshi wanane  Chad.

Magaidi wa Boko Haram waua wanajeshi wanane Chad.

Shambulizi la wanamgambo wa kundi la kigaidi la Boko Haram limeua wanajeshi 8 wa Chad katika eneo la Ziwa Chad katika shambulio ambalo lilijibiwa na wanajeshi hao na kuua wanamgambo 48. Habari hiyo imethibitishwa na msemaji wa jeshi la Chad, Kaiga Kindji aliyesema kuwa, magaidi wa Boko Haram walishambulia maeneo ya jeshi la Chad mapema [&hellip

Mafuriko Nigeria yauwa watu 199; mamia wakosa makazi.

Mafuriko Nigeria yauwa watu 199; mamia wakosa makazi.

Mafuriko yaliyoyaathiri maeneo mengi ya katikati na kusini mwa Nigeria yamesababisha vifo vya watu 199 hadi sasa. Hayo yameelezwa na Idara ya Kukabiliana na Majanga ya nchi hiyo. Mafuriko ya mwaka huu nchini Nigeria yameathiri theluthi moja ya majimbo 36 ya nchi hiyo tangu mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka huu na kusibu watu milioni 1.92 [&hellip

Saudi Arabia yaua raia 79 Yemen masaa 48 yaliyopita.

Saudi Arabia yaua raia 79 Yemen masaa 48 yaliyopita.

Duru za usalama na hospitali nchini Yemen zimeripoti kuwa ndege za kivita za Saudi Arabia zimeua raia wasiopungua 79 katika kipindi cha masaa 48 yaliyopita katika mkoa wa al Hudaydah pekee. Mauaji hayo yamefanyika katika mfululizo wa mashambulizi ya anga yanayoendelea kufanywa na ndege za kivita za Saudi Arabia ikisaidiwa na Marekani na Imarati dhidi [&hellip

Watu 50 Wafariki Kwa Ajali Ya Basi Nchini Kenya.

Watu 50 Wafariki Kwa Ajali Ya Basi Nchini Kenya.

Watu 50 wamefariki dunia leo, Oktoba 10, 2018, na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya ajali ya basi la abiria lililokuwa likitokea Nairobi kuelekea Kisumu kuacha njia na kupinduka katika eneo la Fort Tenan, barabara ya Londiani-Muhoroni, Kaunti ya Kericho, Kenya. Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Kericho, James Mogera, basi hilo lilikuwa na watu [&hellip

Gaidi hatari zaidi wa Misri atiwa nguvuni Derna, Libya.

Gaidi hatari zaidi wa Misri atiwa nguvuni Derna, Libya.

Msemaji wa Jeshi la Taifa la Libya ametangaza kuwa, jeshi hilo limemtia nguvuni kinara wa makundi ya kigaidi katika mkoa wa Derna huko kaskazini mwa Libya. Ahmed al-Mismari amesema kuwa, Jeshi la Taifa la Libya linaloongozwa na Jenerali Khalifa Haftar limefanikiwa kumtia nguvuni Hisham Ashmawy, gaidi hatari zaidi wa Misri katika operesheni iliyofanyika mkoani Derna. [&hellip

Upinzani Wajitangazia Ushindi Cameroon.

Upinzani Wajitangazia Ushindi Cameroon.

Mgombea wa upinzani katika uchaguzi mkuu wa Cameroon Maurice Kamto anadai kuwa ameshinda uchaguzi wa urais wa siku ya jumapili licha ya onyo la serikali dhidi ya hatua hiyo. Kamto ambaye ni kiongozi wa chama cha Rebirth of Cameroon (MRC), ametoa wito kwa rais Paul Biya kuachia madaraka kwa amani. Akizungumza na waandishi wa habari [&hellip

Wakimbizi 10 wa Kongo DR wauawa Angola.

Wakimbizi 10 wa Kongo DR wauawa Angola.

Kwa akali raia 10 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wameripotiwa kuuawa nchini Angola katika makabliano baina yao kwa upande mmoja na askari polisi na wananchi wa nchi hiyo jirani kwa upande wa pili. Televisheni ya serikali ya Angola TPA imethibitisha kutokea mauaji hayo lakini inasisitiza kuwa, raia 10 wa Kongo pamoja na askari mmoja [&hellip

Baraza la mawaziri Libya lafanyiwa mabadiliko.

Baraza la mawaziri Libya lafanyiwa mabadiliko.

Waziri Mkuu wa serikali ya maafikiano ya kitaifa ya Libya inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa amelifanyia mabadiliko baraza lake la mawaziri kwa kuteua mawaziri wanne wapya kushika nyadhifa za Wizara ya Mambo ya Ndani, Fedha, Uchumi na Viwanda na Vijana na Michezo. Katika mabadiliko hayo, Waziri Mkuu Fayez al-Serraj amemteua Fathi Ali Bashagha kuwa [&hellip