Tangaza


Luninga ya Ibn ni ya kwanza ya Kiislamu hapa nchini na kwa sasa hurusha matangazo yake kutoka Dar es Salaam, Tanzania. Luninga ya Ibn inatazamwa karibu na wananchi wote wa mkoa wa Dar es Salaam pamoja  na Tanga.

Luninga ya Ibn inarusha matangazo yake yaliyoandaliwa na idara  ya masoko na sehemu kubwa ya idadi ya watu hufuatilia matangazo hayo, sambamba na mipango ya vipindi vya watoto; Sanaa na kazi za mikono; vipindi vya majadiliano kwa lugha ya Kiingereza (hujulikana kama wide angle) na yale ya Kiswahili yajulikanayo kama “MJADALA”; Sinema, Filamu, mihadhara ya Kiislamu; kipindi cha mapishi na kadhalika.

Luninga ya Ibn ni Luninga pekee yenye kutumia njia za ufanisi zaidi katika kutangaza matangazo kwa ajili ya kukuza biashara yako hapa nchini. Kuichagua Luninga ya Ibn kama njia ya matangazo kwa ajili ya biashara yako ni chanzo pekee cha kukusaidia kufikia wateja wako kwa haraka iwezekanavyo.

Sababu ya msingi kwa wewe kuchagua IBNtv kama njia ya matangazo ni kwamba Luninga ya Ibn hurusha matangazo yake katika lugha 3 tofauti yaani (Kiingereza, Kiswahili, Kiurdu-Kihindi-Gujrati) na kusikilizwa na watazamaji mbalimbali na hivyo kukidhi mahitaji ya wasikilizaji wetu wengi.

Kwa nini utangaze na IBNtv

Matangazo yetu yapo kwenye viwango vya chini na ni ya gharama nafuu kwenye Luninga [(Tangazo la kupita kwa mara moja (Scrolling) na tangazo la muda mrefu (full screen)]
Sisi tunatoa nafasi ya ushindani mkubwa kwa wakati uliopangwa kwa ajili ya matangazo.
Idara yetu ya uhariri na matangazo inaweza kulipamba tangazo lako kwa jinsi unavyotaka, na matangazo yetu huruka kwa masaa 24 kwa siku bila shida.

Wasiliana nasi

Huduma kwa wateja kwa simu no: +255 22 2127555 au
Simu: 255 712 928 995
Email: ibntv@raha.com