Algeria yagundua ghala la makombora la makundi ya kigaidi.


Jeshi la Algeria limetangaza kuwa limegundua ghala lenye silaha na zana za vita yakiwemo makombora 11 lililokuwa likimilikiwa na magaidi kusini mwa nchi hiyo.
Wizara ya Ulinzi ya Algeria imetangaza kuwa, jeshi la nchi hiyo pia Alkhamisi ya jana liligundua maficho 11 ya magaidi katika maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo na kunasa silaha na zana nyingine za kivita.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa, mwezi Novemba mwaka huu vyombo vya usalama vya nchi hiyo viligundua maficho 47 ya makundi ya kigaidi ambayo yalikuwa na kilo 20 za mada za kemikali inayotumiwa kutengeneza mabomu.
Awali jeshi la Algeria lilikuwa limetekeleza operesheni ya kukapambana na magaidi kaika maeneo kadhaa ya nchi hiyo na kuangamiza kadhaa miongoni mwao. Magaidi wengine wametiwa nguvuni.
Katika kipindi cha miongo mitatu iliyopita Algeria imekuwa ikisumbuliwa na harakati za makundi ya kigaidi yanayofanya mauaji na kuvuruga usalama na amani nchini humo.

Leave a Comment