Polisi Yazungumzia Video Ya ‘Mgambo’ Akimshambulia Raia.


Saa chache baada ya video kusambaa mitandao ya kijamii ikimuonesha mgambo akimshambulia kwa rungu mwanaume mmoja huku watu wakiamulia bila mafanikio, Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni Murilo Jumanne ameibuka na kulilizungumzia tukio hilo.
Kamanda Murilo ameeleza ni kweli tukio hilo limetokea eneo la Bunju, ambapo askari mgambo wa jiji watatu walimshambulia mfanyabiashara Robson Orotho baada ya kukataa kulipa faini ya sh 50000/- ya usafi. Orotho, 41, amepigwa na kusababishiwa maumivu makali kwenye maeneo ya mabega, miguu na kichwani, na baadaye kukimbizwa Hospitali ya Mwananyamala kwa matibabu.
Kamanda Murilo ameeleza kuwa tayari Jeshi la Polisi linawashikilia askari mgambo hao watatu ambao ni Kelvin Edson, Gudluck Festo na Rehema Nyange, na watafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo. Aidha, Kamanda Murilo ametoa wito kwa vyombo vya umma na visivyo vya umma kufanya kazi kwa kufuata misngi ya sheria, taratibu na kanuni za nchi.

Leave a Comment