Mamia wajitokeza uzinduzi wa flyover Tazara.


Dar es Salaam. Mamia ya wananchi wamejitokeza kwenye sherehe za uzinduzi wa daraja la juu ‘flyover’ la Mfugale lililopo katika eneo la Tanzara jijini Dar es salaam.
Daraja hilo linazinduliwa rasmi leo Septemba 27, 2018 na Rais John Magufuli.
Viongozi wengine walio hudhuria katika sherehe hiyo ya uzinduzi ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salam , Paul Makonda, katibu Mkuuwa CCM, Dk Bashiru Ally, Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshida, Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Miundombinu, Seleman Kakoso, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage na mwakilishi wa shirika la Jica, Toshio Nagase.

Leave a Comment