Serikali Yabuni Mbinu Mpya Upimaji Ukimwi


Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Ummy Mwalimu amesema kuwa kwa sasa wameweka mkakati wa kuhakikisha mtu anayetaka kujipima mwenyewe anajipima mbele ya mtoa huduma wa afya. Alisema, hayo ni mapendekezo ambayo wameyatoa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Dk Adelardus Kilangi na kwamba watakuja kuwaona wabuge waunge mkono suala hilo.
Mwalimu aliyasema hayo bungeni jana wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu,Suzan Lyimo (Chadema) ambaye alihoji kuwa kutokana na wananchi kuelelimika ni kwa nini serikali hairuhusu watu wajipime wenyewe kwa kutumia kipimo cha Rapid HIV AIDS kwa sababu wakienda vituo vya afya usiku wanakuta vimefungwa wakati kuna watu wanapenda kufanya hilo jambo haraka haraka. Akijibu swali hilo, Mwalimu alisema kwa mujibu wa sheria ya Ukimwi, upimaji unafanyika katika kituo cha Afya lakini wameanza mchakato ndani ya serikali ya kufanya mabadiliko ya sheria ya Ukimwi ili sasa watu waweze kujipima wenyewe.

Mwenyekiti wa kamati namba moja ya Bunge Maalumu la Katiba, Ummy Mwalimu akiwasilisha taarifa ya kamati yake mjini Dodoma jana. Picha na Silvan Kiwale

Leave a Comment