Sakata la Wizi wa Makontena Watuhumiwa 12 Washikiliwa na Jeshi la Polisi.


 

 

dci

Jeshi la Polisi nchini limesema zaidi ya watuhumiwa 12 wamekamatwa kufuatia uchunguzi unaofanywa na wataalamu waliobobea katika uchunguzi wa makosa ya uhalifu wa kifedha wa jeshi hilo, kufuatia agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa dhidi ya wahusika wa wizi wa makontena 329 katika bandari ya Dar es salaam

 

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam,Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai CP Diwani Athuman

amewataja watuhumiwa watano wanaoshikiliwa kuwa ni pamoja, Tiagi Masamaki, ambaye ni Kamishna wa Forodha na Ushuru wa TRA, Habib Mponezia,ambaye ni Meneja wa Kitengo cha Huduma za Ushuru na Eliachi Herieli Mrema,Msimamizi Mkuu wa ICD – Azam.

 

Wengine ni bwana Haroun Mpande wa Kitengo cha Mawasiliano ya Kompyuta ICT – TRA na Khamis Ally Omary ambaye ni Mchambuzi Mwandamizi wa masuala ya Biashara TRA.

 

Hata hivyo,Mkurugenzi huyo wa makosa ya Jinai hakuwataja watuhumiwa wengine saba wanaoshikiliwa na jeshi hilo kutokana nan sababu za upelelezi, ambapo amesema wanatarajia kukamilisha uchunguzi mapema iwezekanavyo na kuwafikisha mahakamani mara moja.

 

Novemba 27 mwaka huu,Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa alifanya ziara ya kikazi ya kushtukiza katika bandari ya Dar es salaam ambapo alibainisha wizi wa makontena 329 ya bidhaa mbalimbali.Kufuatia wizi huo, Waziri Mkuu aliliagiza jeshi la Polisi kufanya uchunguzi na kuwakamata wote waliohusika na wizi huo.

1 Comment

  1. ismail Hussein says:

    Niwakati muafaka kwa Rais wetu na serikali mpya kuona kwamba ina kila sababu ya kutatua kero zinazo wakera wananchi kwa muda mrefu zinazo sababishwa na baadhi ya watendaji wake hasa wenye dhamana ya kukusanya mapato ya taifa na wafanyao ubadhilifu wa matumizi yasiyokuwa na lazima hasa wakiyafanya kwa faida yao,tumeona jinsi baadhi ya maofisa wakikutwa na mali zi sizo kifani kwa uchache hii nihatari kwa ustawi wa taifa letu na watu wake ukizingatia kuwa pengo la walicho nacho na ambao hawana limezidi kuwa kubwa, Heko Rais na tunakuomba uangalie bei za vifaa vya ujenzi kama saruji tunaambiwa kuna wakubwa wameongeza asilimia zao na kusababisha ngarama ya saruji kuwa kubwa hivyo tunaomba uwaulize ni gharama gani inayosababisha saruji kuuzwa 15,0000= kwa mfuko wa50 kg?

Leave a Comment