Zuma asema Nato ina lengo la kubadili utawala huko Libya


Zuma asema Nato ina lengo la kubadili utawala huko Libya

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amesema kuwa muungano wa kijeshi wa Nato unastafidi na azimio nambari 1973 la Umoja wa Mataifa kutekeleza njama yake ya kuubadili utawala ulioko madarakani huko Libya. Zuma amesema wanaamini kwa nguvu zote kuwa azimio hilo linatumiwa vibaya na Nato ili kubadili utawala, kuendesha mauaji ya kisiasa na kuimarisha ukaliaji mabavu wa vikosi vya kigeni huko Libya. Rais wa Afrika Kusini ameitembelea Libya mara mbili tangu mwezi Machi mwaka huu kwa niaba ya Umoja wa Afrika katika juhudi za kutafuta suluhisho la kisiasa kwa mgogoro wa nchi hiyo. Rais Zuma amesema mashambulizi ya Nato yamerudisha nyuma juhudi za umoja huo za kutatua mgogoro wa Libya kwa njia za kidiplomasia. Rais wa Afrika Kusini amesema anatumai kwamba taarifa ya AU itakayowasilishwa leo kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa itafungua njia ya kufikiwa makubaliano ya kutatua mgogoro wa Libya.

3 Comments

  1. May Allah reward you for this nice effort. Students should know basic religious truths and should be able to distinguish the assortment that exists in each belief system that surrounds them.

Leave a Comment