Vikao vya Furaha


Kwa hakika kati ya vikao vingi vinavyowekwa hupatikana maswali chungu nzima kuhusiana na suala hili, ni vikao vya furaha ambavyo huwekwa kwa matukio mbalimbali ambapo watu hupata burudani kama vile sherehe za ndoa, kuzaliwa watoto, n.k.

Swali: Kuna hukmu gani kuhusu vikao hivyo? Ni madhumuni gani ambayo hufaa kuangaziwa katika vikao hivyo? Na upi wigo ambao sheria imeweka ili kuhifadhi hilo? Je! Ni matumizi gani ambayo sheria imeruhusu, au imekataza mambo gani ndani ya vikao hivyo au nje ya vikao hivyo?

Jibu: Maswali hayo na yale yanayofanana na hayo ni kati ya maswali mengi ambayo tutajaribu kuyatolea majibu katika kitabu hiki. Tunamuomba Mola Muweza atie furaha nyoyo za waumini, na tusiwe na huzuni Siku ya Qiyama, siku ambayo haitomfaa mtu mali wala watoto ila mwenye kwenda kwa Mwenyezi Mungu hali ya kuwa moyo wake umesalimika.
Kimetolewa na kuchapishwa na:
Alitrah Foundation
S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania
Simu: +255  22  2110640
Simu/Nukushi: +255  22  2127555

Leave a Comment