Maswali na Majibu


Kitabu hiki kidogo kiitwacho Maswali na Majibu kimekusanya baadhi ya majibu ya maswali aliyoulizwa mtunzi katika hadhara na vikao kadhaa mbalimbali ambavyo alishiriki kujibu maswali hayo. Kisha kamati maalumu ikakaa na kuandaa na hatimaye kuwa kitabu. Hivyo, kimeandaliwa kwa muhtasari sana pamoja na kutaja vitabu rejea vinavyotegemewa zaidi na Ahli Sunna ili watu wengi wapate faida.

Matumaini yetu ni kwamba baada ya mpendwa msomaji kusoma na kuelewa vizuri utawafikishia wengine, na iwapo utapatikana utata au kutofahamika baadhi ya mambo unaweza kuwasiliana nasi. Matarajio ya hapo baadaye ni kujibu maswali hayo na yanayofanana na hayo kwa mapanana marefu na ufafanuzi zaidi.

Kimetolewa na kuchapishwa na:
Al-Itrah Foundation
S.L.P. – 19701,
Dar es Salaam, Tanzania
Simu: +255 22 2110640
Simu / Nukushi: +255 22 2127555

Leave a Comment